Bado Ile tabia ya wanawake kudhaniwa ni
wanaume bado inaendelea michezoni na safari hii imemkuta mwanasoka wa
Equatorial Guinea Genoveva.
Mbaya zaidi ni kwamba Genoveva alikutwa na
kadhia hii toka kwa Waafrika wenziwe ambao ni viongozi wa mamlaka kuu za soka
Afrika ambao walidhani binti huyu anadanganya kuhusu jinsia yake ya kike.
Mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya
Equatorial Guinea alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa ili kuthibitisha kuwa
ni msichana na si mvulana kama ilivyokuwa inahofiwa na hii ni kutokana na nguvu
ambazo anazo akiwa uwanjani na ubora alioonyesha.
Akizungumza na vyombo vya habari Genoveva
alisema alidhani uthibitisho wa jinsia hufanywa hospitalini lakini cha
kushangaza ni kwamba alilazimishwa kuvua nguo na kukaguliwa jambo ambalo
anakiri kuwa lilimsababishia fedheha na hasira.
Kashfa hii ilianzishwa kwenye muichuano ya
kombe la mataifa ya Afrika kwa kina mama ambapo viongozi wa Ghana, Nigeria na
Afrika Kusini walizusha hoja kuwa wachezaji watatu wa Equatorial Guinea ni
wanaume na si wanawake.
Hofu hii iliondolewa baada ya
wachezaji hawa kukaguliwa na kugundulika kuwa ni wanawake halisi
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment