Lionel Messi
Mchezaji mashuhuri, Lionel Messi anasema bado ataendelea
kuwepo katika klabu ya Barcelona baada ya kukanusha uvumi kwamba yuko njiani
kuondoka Barceola.
Messi ambaye ni mshambuliaji wa Barcelona anasisitiza
kwamba hataki kuondoka Barcelona na kusisitiza kuwa madai ya kutaka kocha Luis
Enrique, afukuzwe kazi si ya kweli. Taarifa za awali zilisema mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 27 alitaka sana kuondoka katika klabu hio kufuatia tofauti
yake na kocha Enrique.
Messi, amekuwa akicheza Nou Camp, kwa miaka mingi huku
akishinda mataji mengi. Awali rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu,
alionekana kuzima uvumi huo baada ya bosi huyo kusema Muargentina huyo ana
furaha kubwa klabuni hapo na atabakia hapo hadi mwisho wa mkataba wake mwaka
2018.
Wakati huohuo, kocha Enrique amekana kuwekwa kitimoto
na Bodi ya Wakurugenzi na amesisitiza kwamba hana matatizo yoyote na Messi wala
na mchezaji mwingine yeyote.
0 comments:
Post a Comment