Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya soka ya
Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo ( pichani juu ) kwa mara nyingine
tena amembwaga mpinzani wake mkubwa, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ajentina
na FC Barcelona ya Hispania, Lionel Messi baada ya usiku wa kuamkia leo
kutangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka 2014 wa FIFA, maarufu Fifa Balon
D'Or.
Katika kinyang'anyiro hicho kilichofanyika mjini Zurich, Uswisi, Ronaldo alikuwa anachuana na Messi pamoja na mlinda mlango mahiri wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich, Manuel Neuer.
Ronaldo akiiangalia tuzo yake baada ya kukabidhiwa na mchezaji wa zamani wa
timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry.
Wolfsburg's German midfielde Nadine Kessler ( katikati ) akizungumza machache
baada ya kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa kike kwa mwaka 2014 wa FIFA
Tuzo ya kocha bora wa mwaka 2014 wa Fifa alikwenda kwa Joachim Low toka
Ujerumani.
Rais wa Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, Sepp Blatter akizungumza wakati
wa utoaji wa tuzo hizo mjini Zurich.
0 comments:
Post a Comment