Image
Image

Komla kuenziwa kwa tuzo ya heshima baada ya mwaka mmoja BBC



BBC imeanzisha tuzo za kumuenzi kwa heshima aliyekuwa mtangazaji wake Komla Dumor,mwaka mmoja baada ya kifo chake akiwa na umri wa miaka arobaini na mmoja.

Komla Dumor alikuwa ni mtangazaji wa kipekee aliyekuwa na kipaji cha tofauti mwenye asili ya Ghana,na katika kipindi kifupi cha uhai wake alifanya kazi ya kutukuka na kuacha athari zake Afrika na dunia kwa ujumla.

Tuzo hiyo endapo atapatikana mshindi,basi itakwenda kwa mtu anayefanya kazi na kuishi barani Afrika,ambaye anauzoefu mkubwa katika kazi ya uandishi wa habari,na uwezo wa kipekee wa kuwasilisha habari kutoka barani Afrika.

Na mshindi wa kinyang'anyiro hiki atajishindia muda wa miezi mitatu kufanya kazi na BBC mjini London.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment