Siku chache baada ya mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kufuta
usajili wa Dawa aina tano na kuzuia uingizaji,uuzaji na matumizi yake ,
wafamasia wauzaji wamesema hatua hiyo imechelewa na kuitaka
mamla hiyo kuweka mikakati thabiti ya kufanikisha zoezi hilo ambalo linalenga
kunusuru maisha na afya za watanzania.
Wamesema wamekuwa wakilalamikia Dawa
hizo na kutoa ushauri kwa kipindi kirefu huku wakieleza wasiwasi wa baadhi ya
wauza Dawa kutokuwa waaminifu na kuendelea kuzizungusha sokoni kama
wanavyofanya kwa Dawa zilizokwisha muda wake.
Kwa upande wa wamiliki wa maduka
ya Dawa nchini pamoja na kueleza TFDA kuwashirikisha kikamilifu kabla ya
kutangaza rasmi hatua hiyo wameitaka pia kuwekeza katika matangazo kwa vyombo
vya habari na mabango na kuchukua hatua stahiki kwa watao kaidi amri hiyo
kutokana na kubainika kuwa na athatri mbaya zaidi kwa afya na maisha ya Binadamu.
0 comments:
Post a Comment