Wananchi
wa vijiji viwili vya loto na seloto wilayani babati mkoani manyara wameitaka
kamati ya kudumu ya bunge,kilimo, mifugo na maji kuunda tume ya kuchunguza
miradi ya maji ukiwemo ule wa visima miradi ya vijiji 10 inayofadhiliwa na
benki ya dunia katika halmashauri ya wilaya ya babati kwa kuwa imeonyesha
kuuwepo kwa usiri na kujengwa chini ya kiwango,sanjari na hilo
wakiilalamikia kuundiwa bodi ya maji kwa nguvu ambayo imekuwa haitoi taarifa za
mapato na matumizi kwa miaka mitatu sasa.
Malalamiko
hayo wameyatoa kwa kamati hiyo iliyofika kata ya dareda katika ziara ya
ufuatiliaji wa miradi ya maji na kuangalia thamani ya fedha kupitia mpango wa
matokeo makubwa sasa(THE BIG RESULT NOW) na hapo ndipo wananchi hao walipotupia
lawama halmshauri hiyo kuwaunganisha miradi mitatu ya
maji ya water,aid,mradi wa kanisa katoliki-(DMDD)na ule wa benki ya dunia
kuwepo katika mtandao mmoja,aidha kutokushirikishwa na kuhoji miradi ya
wafadhili huku pia wakitishia kuacha kulipa maji kwa mfumo wa mita
na kuikataa bodi iliyopo.
Hata
hivyo mkurugenzi wa maji mijini kutoka wizara ya maji BI MARY MBOWE akitolea
ufafanuzi wa mgogoro huo uliopo kati ya wananchi hao na halmashauri hasa pale
walipomtaka mkurugenzi huyo kutambua kuwa watalipia maji hayo endapo kamati zao
zitasimamia miradi hiyo.
Akitoa
msimamo wa kamati ya kudumu ya Bunge ya maji kilimo na mifugo,mjumbe wa kamati
hiyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la babati vijijini BW JITU VRAJILAL SONI ameiagiza
ofisi ya katibu tawala mkoani manyara kwa kushirikiana uongozi wa
bonde la kati utoa elimu ya uundwaji wa vyombo vya maji na juu ya usimamizi wa
raslimali maji ili kuondoa mgogoro huo wa muda mrefu.
Kamati
hiyo ya kudumu ya bunge imefanya ziara katika vijiji hivyo viwili vya loto na
seloto kufuatia miezi michache iliyopita wananchi wa vijiji hivyo waliandamana
kupinga kunyimwa taarifa za mapato na matumizi ya miradi hiyo ya maji,aidha pia
wakilalamikia hofu iliyopo ya matumizi makubwa ya fedha katika mradi wa
visima unaofadhiliwa na benki ya Dunia.
0 comments:
Post a Comment