MAMLAKA ya hali
ya hewa nchini (TMA), imewataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua
kubwa inayotarajiwa kunyesha katika maeneo ya Ukanda wa Pwani.
Taarifa
iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mamlaka hiyo, ilisema mvua hiyo itanyesha kwa
zaidi ya milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Januari 18 hadi 20 mwaka huu.
Maeneo ambayo
yataathirika na mvua hizo ni Mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani,
Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja, Zanzibar.
"Hali hii
inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa eneo la Bahari ya Hindi
Mashariki mwa Kisiwa cha Madagasca hivyo kusababisha ongezeko la unyevunyevu
kutoka misitu ya Congo," ilifafanua taarifa hiyo.
Kutokana na hali
hiyo, wakazi waishio katika maeneo hatarishi kama mabondeni ni vyema wakachukua
hatua zinazostahili ili kuepuka madhara.
0 comments:
Post a Comment