Mtuhumiwa wa wizi wa rediokoli ya kituo cha polisi
cha Litembo wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma Bosko Ndunguru (40), amefariki akiwa
mahabusi na kitanzi shingoni.
Mwili wake ulikuwa unaning’inia kwenye dari ya mahabusi kituo cha polisi Mbinga mjini akidaiwa ni baada ya kujinyonga kwa shati alilokuwa amelivaa hapo awali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela , alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1.00 asubuhi.

Msikhela alidaiwa mwaka jana Ndunguru anatuhumiwa kuvunja kituo cha polisi cha Kijiji cha Litembo na kuiba redio koli ya kituo hicho na kutoroka lakini baadaye alikamatwa.
Alisema kabla ya kujiua ilidaiwa alilalamika kuwa jamaa zake hawampendi jambo ambalo liliwashangaza mahabusu wenzake.
Alisema polisi kwa kushirikiana na Mganga Hospital ya Wilaya ya Mbinga waliuchunguza mwili wa Ndunguru na kuthibitisha kuwa chanzo cha kifo ni kujinyonga na kwamba na jamaa zake walikabidhiwa mwili huo.
0 comments:
Post a Comment