Image
Image

Rais Kikwete apangua baraza la mawaziri na kuweka sura mpya bila kupoteza muda


Rais Jakaya Kikwete amepangua Baraza la Mawaziri jana jioni na kuweka sura mpya huku akiwaapisha chapu chapu, hatua iliyokuja muda mfupi  baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu mchana.
Wateule hao wanaelekea Dodoma kesho tayari kwa kikao cha Bunge kinachoanza keshokutwa. 
Mabadiliko haya ambayo yamekuwa ya kushtukiza kwa vyombo vya habari, yamekuwa ya aina yake Pale Rais alipoteua na kuapisha papo kwa papo.
Uteuzi mpya ni kama ifuatavyo:
MANAIBU MAWAZIRI WAPYA
Anna Kilango ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akichukua nafasi ya Jennister Muhagama.
Charles Mwijage  ambaye ni  Mbunge Muleba Kaskazini ameteuliwa kuwa Naibu Waziri  Nishati na Madini.
MANAIBU AMBAO SASA NI MAWAZIRI KAMILI
George Simbachawene sasa  Waziri wa Nishati na Madini, zamani  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini akifanyakazi na Profesa Muhongo.
Hata hivyo mwaka jana alihamishiwa Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Jennista Muhagama zamani, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi sasa Jenista Mhagama Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uratibu na Bunge
MAWAZIRI WALIOBADILISHWA
Steven Wasira zamani Ofisi ya Rais Mahusiano na Bunge sasa Kilimo na Chakula (aliwahi kushika wadhifa huo).
Christopher Chizza zamani Wizara ya Kilimo,  sasa Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu  Uwezeshaji na Uwezekazaji
Dk. Harrison Mwakyembe zamani Uchukuzi sasa Afrika Mashariki Samuel Sitta zamani Afrika Mashariki sasa Uchukuzi.
William Lukuvi zamani Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera , Uratibu na Bunge sasa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Dk. Mary Nagu,  zamani Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji sasa Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu.
MANAIBU WALIOBADILISHWA
Ummy Mwalimu  zamani Ofisi ya Makamu Rais Mazingira sasa  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Stephen Masele zamani Nishati na Madini sasa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mzingira.  
Angella Kairuki zamani Naibu Sheria na Katiba sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
WIZARA ZILIZOPANGULIWA
Wizara ya Uchukuzi, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kilimo na Chakula, Nchi ofisi ya Rais mahusiano na uratibu, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uratibu wa Bunge. Nyingine hazikuguswa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment