Kasumba ambayo imekuwa ikijengeka
mara nyingi na inazidi kujengeka kwa
wanafunzi mbali mbali nchini juu ya inapofikia kipindi cha kupiga kura katika
uchaguzi mkuu hatimaye inaelezwa kuwa zaidi ya wanafunzi laki sita wa vyuo
vikuu, vyuo vya kati na kidato cha nne nchini huwenda wasishiriki katka zoezi
zima la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao wa madiwani,wabunge na Rais
kutokana na ratiba ambayo imetolewa na wizara ya elimu kuhusu mihula ya kufunga
na kufungua vyuo nchini kukinzana na ratiba ya tume ya uchaguzi nchini, NEC.
Kutokana na hofu hiyo, CHASO imeandikia waraka na kuelekeza katika
ofisi ya katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ikimtaka
kuwatumia wabunge wake kupeleka hoja binafsi Bungeni ya kurekebisha sheria ya
uchaguzi ili iwaruhusu watanzania wote kupiga kura wakiwa mahali popote ndani
ya mipaka ya Tanzania.
Ratiba ya mihula ya kufunga na kufungua vyuo
ambayo imetolewa na wizara ya elimu mwaka huu, imeibua hofu kwa wasomi wa vyuo
mbalimbali nchini kutoshiriki ipasavyo kwenye uchaguzi mkuu ujao, ambapo
jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa chama cha demokrasia
na maendeleo(CHASO) Mkoani Mbeya wamelibaini hilo na kuanza kupaza sauti zao
kuidai haki hiyo.
0 comments:
Post a Comment