Image
Image

Taqwa lanaswa na shehena ya magendo, likitokea harare kwenda Dar abiria wasota kwa zaidi ya saa 6 mbeya.

Baadhi ya bidhaa za magendo zikiwa zipo karibu na viti vya gari la Taqwa
Zaidi ya abiria 60 ambao walikuwa wakisafiri kutoka harare nchini zimbwe kwenda jijini Dar es salaam wamekwama jijini mbeya kwa zaidi ya saa sita,baada ya basi lenye namba za usajili T776 CRN mali ya kampuni ya TAQWA walilokuwa wakisafiria kukamatwa likiwa limebeba bidhaa mbalimbali za magendo zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 39.
Juu ni box ambazo zilikuwa na bidhaa za magendo na chini ni chupa za vimiminika zilizokamatwa katika kadhia hiyo.
Msako wa kushtukiza katika vyombo vya usafiri ambao umefanywa na mamlaka ya chakula na Dawa, TFDA, na mamlaka ya mapato tanzania, TRA, kwa kushirikiana na jeshi la polisi ndio ambao umelinasa basi hilo likiwa limesheheni bidhaa za aina mbalimbali yakiwemo maziwa ya watoto aina ya LACTOGEN ambayo hayajasajiliwa nchini na hivyo kuhatarisha afya na maisha ya watanzania.Bofya hapa kufahamu>>http://www.itv.co.tz/news/local/1588-16784/Basi_la_Taqwa_lanaswa_na_shehena_ya_magendo_likitokea_harare_kwenda_Dar.html
Bidhaa ambazo zimekamatwa zikionekana hapo.

 




 





Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment