Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN amewaongoza Watanzania katika
kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika
uwanja wa Aman Zanzibar.
Mara baada ya Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN kuwasili uwanja wa
Aman alipokea heshima ya mizinga 21 kabla ya kukagua gwaride lililoandaliwa na
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania -JWTZ kwa kushirikiana na Vikosi vya
SMZ.
Baadaye alipokea maandamano ya
wananchi kutoka mikoa mitano ya Zanzibar yaliyoongozwa na wananchi waliobeba
picha za marais na wenyeviti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar waliotangulia.
Maandamano hayo yalifuatiwa na
gwaride la vikosi vya JWTZ na Vikosi vya SMZ ambalo lilitoa heshima mbele ya
mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI
MOHAMMED SHEIN kwa mwengo wa pole na mwendo wa haraka.
Sherehe hizo ambazo zilipambwa
kwa burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya, pia
zilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta JAKAYA KIKWETE,
viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa, mabalozi na wageni waalikwakutoka ndani na nje ya nchi.
Ilikuwa Januari
12 mwaka 1964 wanapinduzi wa Zanzibar
wakioongoz wa na Mzee ABEID AMMAN
KARUME kwa kitumia silaha za jadi , wali
uondoa madarakani utawala wa s ultani wa Zanzibar na kuifanya iwe huru.
Miezi mitatu baadaye ilipofika
Aprili 26 , mwaka 1964 Zanzibar huru
iliungana na Jamhuri ya Tanganyika na kuunda
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment