Tafiti zinaonyesha zaidi ya tani laki nne za mahindi na
mpunga zenye uwezo wa kulisha
watu milioni 2 hupotea kila
mwaka kutokana na kuharibiwa na
panya mashambani kabla ya kuvunwa.
Hayo yameelezwa mkoani Morogoro na watafiti wa sayansi kutoka nchi
za Tanzania, Uganda na Ubelgiji wakati wa
ufunguzi wa mradi mkubwa utakaohusisha wataalam kwa kushirikiana na
wananchi katika kupunguza tatizo la
panya kuharibu mazao.
Kwa sababu hiyo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine SUA
Profesa GERALD MONELA amewataka watafiki kushirikisha wakulima ipasavyo ili
waweze kusaidia kupata ufumbuzi wa
kuzuia upotevu wa vyakula unaosababishwa na panya.
Mradi wa utafiti wa panya
unalenga kusaidia kupunguza madhara na
gharama kwa wakulima wanaolazimika
kutumia sumu kuua panya
mashambani ambapo wanaweza kutumia njia za kiikolojia kuua panya bila
kusababisha madhara kwa viumbe wengine.
0 comments:
Post a Comment