Image
Image

Tanzania kudumisha uhusiano na Msumbiji



Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amehudhuria kuapishwa Rais wa tano mpya wa msumbiji Felipe Nyusi na kusisitiza kuendelea kuimarishwa uhusiano baina ya nchi mbili hizo.

Nyusi aliapishwa rasmi jana mjini Maputo kuanza kuongoza kama rais wa 5 wa Msumbiji.  

Kikwete amesema alipozungumza na Rais Nyusi kwamba uhusiano wa Tanzania na Msumbiji ni wa kidugu kwa hivyo utaendelea kudumishwa kwa manufaa ya pande mbili.

Felipe Nyusi ameingia madarakani akimrithi rais Armando Guebuza baada ya kujinyakulia asilimia 57 ya kura na kumwangusha mpinzani wake kiongozi wa chama cha Renamo Alfonso Dhlakama katika uchaguzi wa rais uliofanyika Oktoba 15 mwaka jana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment