Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya
Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akionyesha gazeti la
"Tuwasiliane" linalochapishwa na UTPC na kusambazwa kwa wadau na
maeneo mbalimbali ya jijini Mwanza kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini, Alvaro Rodriguez aliyetembelea makao ya ofisi hizo kwa ajili ya
mazungumzo na kuboresha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa Umoja huo wa
vilabu vya waandishi wa habari nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya
Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akizungumza na Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mshauri wa
masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi wa UN Tanzania, Bi.
Chitra Massey (kulia) alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo jijini Mwanza.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akichangia jambo wakati wa mazungumzo
na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC)
Abubakar Karsan makao makuu ya ofisi za umoja huo jijini Mwanza
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi
wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan wakati wa mazungumzo ya kuboresha mahusiano
baina ya mashirika ya umoja wa mataifa na umoja wa vilabu vya waandishi wa
habari nchini Tanzania.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment