Siku ya jana January 12 Naibu Waziri wa Wizara ya
Fedha alikuwa katika mahojiano kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV,
hapa kuna kile alichokizungumza kuhusu ishu ya nini kifanywe kuwabana wakwepa
kodi na wala rushwa, msimamo wake kugombea Urais 2015 na ishu ya wahusika
waliochukua Fedha za Escrow.
“Kwa
nchi yetu, upande mmoja wa hili la kukwepa kodi na upande wa rushwa ukitaka
kukomesha na lenyewe linasubiria Katiba Mpya tutakapokwenda kwenye Sheria
hili tutasimamia mpaka koo litakauka… Yaani mtu kupokea rushwa anatakiwa anatakiwa
akikadiria hivi siku nikipokea rushwa nikikamatwa madhara yake ni nini…“–
Mwigulu Nchemba.
Anatakiwa
ajue siku ileile kwamba hakuna dhamana, taratibu za kimahakama zitaendelea
akiwa ndani nakutoka hapo adhabu yake inatakiwa imtishe… Kama mtu amesababisha
hasara ya bilioni thelathini, kama adhabu nii kumuondoa tu kwenye nafasi
aliyokuwa nayo umempa likizo akatumie fedha… Umempa send-off akasherekee fedha
ya umma…”– Mwigulu Nchemba.
Kuhusu
hatua ambazo zimefikiwa mpaka sasa kwa wale waliochukua pesa za Escrow,
Naibu Waziri huyo alisema; “Taarifa nilizonazo tayari Mamlaka ya Mapato
imeshafanya hesabu… Kuhusu haya mambo ya Kodi kweli tumedhamiria, kwamba lazima
kodi ilipwe na hili si jambo la mjadala… Hatuwezi tukasamehe kodi kubwa vile
halafu tukakimbizana na mama anayeuza mchicha…”– Mwigulu Nchemba.
Alipoulizwa
kuhusu msimamo wake kwenye Uchaguzi 2015 alijibu; “Ninataka nifocus sana kumsaidia Waziri kwenye haya
majukumu ambayo tumepewa na Mheshimiwa Rais kuhakikisha kwamba Serikali
inatimiza wajibu wake… Nikirudi kwenye Chama namsaidia Katibu Mkuu kusimamia
misingi ya Chama… Nisingependa niwe miongoni mwa wanaovunja miiko.. Tutavuka
mto tukishafika mtoni kufuatana na taratibu zetu…”Mwigulu Nchemba.
Msimamo wangu kwenye masuala ya msingi yanayohusu
taifa letu huwa hauyumbi wanaonifahamu wanajua.
Millard ayohttp://millardayo.com/mwigulu-onitv-jan12/
Millard ayohttp://millardayo.com/mwigulu-onitv-jan12/


0 comments:
Post a Comment