Watu wanaosadikiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha wamevamia fukwe
kwa kasi na kufukia kina cha bahari kwa kujenga nyumba za kisasa licha ya
kuwepo kwa sheria ya mazingira na mipango miji zinazozuia ujenzi wa nyumba
umbali ya mita sitini toka katika kina cha maji katika maeneo fukwe za bahari.
Tambarare Halisi imeshuhidia baadhi ya
majengo mapya yakiwa yamejengwa baada ya kusogezwa kwa kina cha bahari katika
maeneo ya kawe na mbezi beach,ambapo baadhi ya wakazi waoishi jirani na maeneo
hayo wamesema watu wanaofanya uendelezaji huo ni wakubwa kiasi cha mamla
zinazotakiwa kutekeleza sheria hizo zinashindwa.
Akizungumza eneo la tukio mkurugenzi wa ufuatiliaji na utekelezaji wa mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa
mazingira-NEMC Dokta Robert Ntakamulenga
amesema tatizo la baadhi ya taasisi ikiwemo wizara ya ardhi, na manispaa la
kutofuata sheria za mazingira limechangia kuendelea baadhi ya watu kupimiwa
viwanja kihalali katika maeneo fukwe kinyume na sheria ya mazingira.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira
Dokta Binilithi Mahenge alipofika katika eneo fukwe hizo ameshuhudia uvamizi
huo na kukiri kuwa majengo hayo
yanapaswa kubomolewa na kusisitiza hakuna aliyejuu ya sheria na kuahidi
uvunjaji wa nyumba hizo utafanyika muda mfupi baada ya timu iliyounda na waziri
mkuu kushughulikia tatizo hilo itakapo wasilisha taarifa yake.
0 comments:
Post a Comment