Kamati ya bunge ya hesabu za serikali PAC imebaini upotevu wa
fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.5 za mamlaka ya usimamizi wa bandari TPA ambazo
zimetumika lakini nyaraka zake hazionekani huku ikiuagiza uongozi wa mamlaka
hiyo kuhakikisha fedha zote za nyongeza ya posho za safari walizolipwa
watumishi tangu mwaka 2011 kabla msajili wa hazina hajathibitisha zinarudishwa.
Mwenyekiti wa kamati ya PAC Mh Zitto Kabwe ametoa agizo hilo
wakati kamati yake ilipokutana na bodi na uongozi wa TPA baada ya kukagua
vitabu vyake vya mahesabu ambapo amesema licha ya kiwango cha posho zilizolipwa
kuwa kikubwa lakini waliharakisha kujilipa kabla msajili wa hazina
hajathibitisha ambapo afisa wa ngazi ya juu alilipwa shilingi laki tano kwa
siku kwa safari ya ndani ya nchi na ya nje ya nchi dola za kimarekani mia nane.
Akizungumzia suala la ukosefu wa nyaraka za fedha ambazo tayari zimeshatumika
makamu mwenyekiti wa PAS Mh.Deo Philikonjombe amesema tatizo hilo limekuwa sugu
kwa taasisi mbalimbali za serikali hali inayoashiria kuwa kuna baadhi ya
wakurugenzi na watumishi wanafuja fedha za umma kinyume na taratibu na
wanapobanwa wanapeleka nyaraka ambazo wakati mwingine ni za kufoji.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TPA na mhasibu wake mbali na kukiri
upotevu wa nyaraka hizo wamedai kuwa tatizo hilo limetokana na uhifadhi wa
nyaraka ambao hadi leo nyaraka nyingi za TPA zinahifadhiwa kwenye karatasi na
kuiahidi kamati hiyo kuwa wataziwasilisha mwisho wa mwezi wa mwezi febuari
mwaka huu hali iliyozua maswali mengi kwa wajumbe wa kamati hiyo kuwa
watazipata wapi kama kipindi chote hicho hazijaonekana.
0 comments:
Post a Comment