Kasi ya uharibifu wa misitu
ya hifadhi ya safu za mlima mbeya imesababisha zaidi ya vyanzo vya maji 40
kukauka katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, hali ambayo imeushtua uongozi wa
mkoa wa mbeya ambao sasa umebuni mpango wa kuhifadhi mistitu hiyo kwa
kuwashirikisha wadau wote wa mazingira koani mbeya.
Akizindua mpango huo wa
kuhifadhi misitu ya safu za mlima mbeya na kuongoza zoezi la upandaji wa miti
zaidi ya 200 katika kata ya iziwa, mkuu wa mkoa wa mbeya abbas kandoro amesema
mkoa wa mbeya una jumla ya misitu 142 ambayo inahifadhiwa, lakini kati yake
misitu 20 ni muhimu zaidi kutokana na kuwa ipo kwenye vyanzo vya maji
vinavyotegemewa na wakazi wote wa mkoa wa mbeya, hivyo akawataka wananchi wote
kushiriki kuilinda.
Kwa upande wake, afisa mazingira
wa baraza la taifa la mazingira (NEMC), kanda ya nyanda za juu kusini,
nzwamkulu ezekiel amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuhifadhi mazingira na
vyanzo vya maji vya eneo hilo, huku mwakilishi wa bodi ya bonde la maji la ziwa
rukwa, mkwanjilwa watson akitoa wito kwa wananchi kutumia maji kiuchumi ili
waweze kujiletea maendeleo.
Baadhi ya wadau wa mazingira
mkoani mbeya wamesema kuwa mpano huo ukitekelezwa kama ulivyopangwa unaweza
kurejesha uoto wa asili ambao umeanza kutoweka katika safu za milima hiyo na
maeneo mengine.
0 comments:
Post a Comment