Hatimaye
wachimbaji wote watatu waliokufa kwa kufukiwa na kifusi cha jabali katika mgodi
wa dhahabu wa Onesmo Goldmine Mawemeru uliopo katika kijiji cha Nyalugusu
Wilayani Geita imeopolewa jana usiku baada ya juhudi za siku nne.
Hatua hiyo imedaiwa ni matokeo ya ushirikiano
na mshikamano mkubwa uliooneshwa katika kutekeleza zoezi hilo kati ya Uongozi wa
Mgodi huo, wadau na serikali ya wilaya na mkoa zoezi lililokuwa linafanyika
usiku na mchana kwa kushirikisha wadau tofauti na hivyo kufanikiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Kamishna
msaidizi mwandamizi wa polisi Joseph Konyo akithibitisha LEO kupatikana kwa
miili hiyo alisema kazi hiyo ilihitaji ujasiri na kujituma na ndicho
kilichofanyika kuhakikisha miili yote mitatu imeopolewa.Bofya kusoma habari hii kwa kina->http://www.eatv.tv/news/current-affairs/miili-ya-waliofukiwa-kifusi-mgodini-yaopolewa
Amewataja miili yao walioopolewa kuwa ni
Benjamin Yusuph, Robert Edward na Nsulwa Bungila ambao wote walifukiwa katika
mgodi huo Januari 11 saa moja usiku na wengine wanne Samson Haroun, Rutu
William, Faida Bukombe na Seif Ally waliokolewa siku ya tukio.
0 comments:
Post a Comment