Mkazi wa mtaa wa Kitwana kata ya Busoka wilayani
Kahama mkoani Shinyanga Regina Shija
(55) ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga kichwani
na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa Kimapenzi.
Afisa mtendaji wa
Mataa huo, Bw. Rafael Jumanne ameiambia ITV kuwa tukio hilo limetokea juzi
majira ya saa 5.00 usiku ambao watu wasiofahamika walivamia nyumbani kwa Regina akiwa
anajiandaa kulala na wajukuu wake wawili.
Amesema baada ya
watu hao ambao idadi yao haijafahamika, kuvamia nyumbani hapo walianza
kumkatakata mapanga mama huyo kichwani na
mkono wa kulia hali iliyosababisha kuvuja damu kwa wingi baadaye
kufariki dunia.
Afisa Mtendaji
huyo amedai kuwa chanzo cha mauji hayo
bado hakijafahamika ingawa yanahusishwa na wivu
wa kimapenzi na kwamba jeshi la
Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu huyo na kuupeleka
kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya wilaya ya
Kahama.Kwa taarifa zaidi Bofya hapahttp://www.itv.co.tz/news/local/1588-16591/Mwanamke_auawa_kwa_kukatwakatwa_mapanga_kwa_kile_kinachodaiwa_wivu_wa_mapenzi.html
0 comments:
Post a Comment