Image
Image

Kamati ya PAC yacharukaa upyaa yalitaka shirika la utangazaji TBC kuwa na mipango thabiti katika kujiendesha.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma –PAC- imelitaka Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kuhakikisha kuwa linakamilisha mipango ya kuliwezesha shirika kujiendesha lenyewe na kuhakikisha matangazo yake yanasikika nchi nzima.
Agizo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha za Serikali na Mashuirika ya Umma PAC, DEO FILIKUNJOMBE jijini DSM wakati wa kikao kati ya kamati yake na uongozi wa TBC kujadili Hesabu za Shirika hilo kwa mwaka 2012/2013.
Viongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC wamehudhuria kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge Hesabu za Mashirika ya Umma PAC, jijini DSM lengo ikiwa ni kupitia hesabu za TBC na kungalia namna ya kuboresha hali ya kifedha ya TBC ili iweze kujiendesha na matangazo yake kusikika nchini nzima.
Makamu Mwenyekiti wa PAC DEO FILIKUNJOMBE ameiagiza TBC kuhakikisha kuwa inaandaa kikao haraka katika wiki ya kwanza ya Kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza mwishoni mwa Januari mwaka huu, kikao kitakacho shirikisha Kamati tatu za Bunge kwa lengo la kujadili na kumaliza changamoto za kifedha zinazikabili TBC
Kuhusu usikivu FILIKUNJOMBE aliuliza ni kwa nini Matangazo ya TBC hayasikiki katika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na LUDEWA ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA alitoa maelezo ya kina na kusema shirika linajitahidi kuhakikisha linarekebisha maeneo yote ambayo hayasiki vizuri .
Kuhusu kampuni ya magazeti ya serikali Kamati ya PAC, imesema haijaweza kupitia hesabu zake kwakuwa makabrasha ya kampuni hiyo yalicheleweshwa kufikishwa katika kamati hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo DEO FILIKUNJOMBE amesema TSN wataitwa siku nyingine huku akiongeza kuwa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG inaonyesha kuwa kampuni hiyo imepata hati chafu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment