Waziri wa mambo ya ndani wa Senegal amepiga
marufuku usambazaji nchini Senegal wa toleo la wiki hii la jarida la vibonzo la
kila wiki la Charlie Hebdo lililoshambuliwa juma lililopita mjini Paris nchini
Ufaransa.
Kibonzo
cha Mtume Muhammad kimewekwa katika ukurasa wa mbele wa toleo hilo, akiwa na
bango lenye maandishi “Je suis Charlie, tout es pardonné”, ikimaanisha
“mimi ni charlie
nimesamehe yote.”
Shirika
la habari la Senegal limebaini kwamba magazeti ya jarida hilo la Chalie Hebdo
yalipigwa marufuku kuzambazwa nchini Senegal tangu miaka miwili iliyopita,
lakini yanapatikana tu katika baadhi ya maktaba.
Hata
hivyo rais wa Senegal, Macky Sall, aliungana Jumapili Januari 11 mwaka 2015, na
rais wa Ufaransa pamoja na raia wa taifa hilo katika maandamano ya kupinga
mauaji ya watu 12 wakati wa shambulio dhidi ya jarida la vibonzo la Charlie
Hebdo.
Rais wa Senegal, Macky Sall akiwa na rais wa Ufaransa,
François Hollande Januari 11 kabla ya maandamano ya kitaifa, mjini Paris.
Wakati
huo rais Macky Sall alilaumiwa na wanasiasa pamoja na viongozi wa kidini kwenye
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Wengi waliona kwamba kitendo hicho
cha rais cha kuungana katika maandamano hayo ni kufuru, wengine wakiona kuwa ni
kuiunga mkono Ufaransa kwa kuukashifu Uislam.
Toleo
hilo la wiki hii la jarida la vibonzo la kila wiki la Charlie Hebdo
limechukuliwa nchini Senegal kama uchokozi dhidi ya Uislam.
Kwa
mujibu wa chanzo cha wizara ya mambo ya ndani, kama rais Macky Sall
alijielekeza Paris, ni “ kuonyesha heshima kwa maisha ya binadamu”. Na kama
amechukua uamzi wa kupiga marufuku usambazaji wa toleo hilo la Charile Hebdo ni
"kuonyesha heshima kwa imani ya Uislam", kimeendelea
kusema chanzo hicho.
Hata
gazeti lingine la Ufaransa Libération limepigwa marufuku nchini Senegal.
0 comments:
Post a Comment