Chama tawala cha Patrioyoc Front kinauhakika
wa kushinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka
upinzani.
Waangalizi wa kikanda katika uchaguzi huo,
wanasema wameridhishwa na maandalizi ya zoezi zima la upigaji kura.Uchaguzi huo
unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo
kupitia chama tawala na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka United Party
for National Development.
Wagombea wote katika nafasi hiyo ya Urais
wakati wakijinadi wameahidi kuimarisha mfumo wa elimu nchini humo, kutengeneza
ajira. Huku wapiga kura nao wakitumaini kuwa wanasiasa hao watatimiza ahadi
zao.Ikiwa ni miaka 50 toka nchi hiyo ilipojipatia uhuru, Zambia imekuwa imara
na imeendelea na msimamo wake wa kufanya uchaguzi tangu kumalizika kwa siasa za
chama kimoja nchini humo.
Hata hivyo mshindi katika uchaguzi huo wa leo
atatumikia kipindi cha miezi 18 iliyobakia, katika awamu iliyobaki, aliyoiacha
marehemu Michael Sata, wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu
mwakani 2016.
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia
saa 12 kamili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni. Tume ya Uchaguzi nchini Zambia
imesema zoezi la uhesabuji kura, linatarajiwa kuanza muda mfupi tu baada ya
zoezi la upigaji kura kukamilika, huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa katika
kipindi cha saa 48.
BBC
0 comments:
Post a Comment