Leo ni siku ya maandalizi ya timu za taifa za soka za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Cote d'Ivoire kujiandaa kwa mchuano wa nusu fainali,
kuwania taji la ubingwa wa Afrika.
Mechi hiyo itachezwa Jumatano Februari 4
katika uwanja wa Bata nchini Equatorial Guinea kuanzia saa nne usiku saa za
Afrika Maashariki sawa na saa tatu usiku saa za Afrika ya Kati.
Mataifa haya mawili yalimenyana mwaka
uliopita katika mechi ya kufuzu kucheza fainali hizi, DRC walifungwa mabao 2
kwa 1 nyumbani na walipokwenda Abidjan waliwafunga Cote d'Ivoire mabao 4 kwa 3.
Hii ni wazi kuwa mechi haitakuwa rahisi
Jumatano wiki hii, na kocha wa Leopard Florent Ibenge atakuwa anataka
kudhirihisha kuwa ana uwezo wa kuiongoza timu yake kufika fainali, sawa na
Mfaransa Herve Renard ambaye lengo lake ni kuhakikisha kuwa Cote d'Ivoire
inanyakua taji hilo walilonyakua mwisho mwaka 1992.
Nusu fainali ya pili itakuwa siku ya Alhamisi
kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea katika uwanja wa Malabo.
Mshambualiaji wa Ghana, Asamoah Gyan anauguza jeraha.
Mshambualiaji wa Ghana, Asamoah Gyan anauguza jeraha.
0 comments:
Post a Comment