Kamati
ya nidhamu ya Shirikisho la soka duniani FIFA inachunguza ni kwanini mshambuliaji wa timu
ya taifa ya Senegal na klabu ya west Ham nchini
Uingereza Diafra Sakho aliamua kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa
kilichokuwa kinashiriki katika michuano inayoendelea ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Equatorial Guinea.Sakho mwenye umri wa
miaka 25 alisema alijiodoa katika kikosi cha Senegal kwa sababu ya jeraha la
mgongo lakini alioneakana akichezea klabu ya West Ham na kuifungia wakati wa
mchuano wa kuwania taji la FA dhidi ya Bristol City, mchuano ambao West Ham ilipata ushindi wa bao moja kwa bila, bao
lililofungwa na mchezaji huyo.Sheria za FIFA zinaeleza kuwa mchezaji hawezi kuichezea klabu yake, wakati akihitajika
kuichezea timu yake ya taifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment