Bondia wa ngumi za kulipwa Tanzania, anayeshikilia mikanda lukuki ikiwemo wa WBF,
Francis Cheka, amehukumiwa kwenda jela
miaka mitatu, sambamba na kutakiwa kulipa shilingi milioni moja kama gharama za
matibabu na fidia, baada ya kupatikana na hatia ya shambulio la kudhuru mwili
dhidi ya meneja wa baa yake ya vijana social, bahati kabanda,mkazi wa morogoro.
Hukumu hiyo
imetolewa na hakimu mkazi mwandamizi katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa
morogoro, said msuya, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi
wanne wa upande wa mashtaka, ambapo bila shaka umemtia hatiani mshtakiwa kama
alivyokuwa akishtakiwa ambapo hakimu msuya amedai kutoa adhabu hiyo ili iwe
fundisho kwa mshtakiwa na wegine wanaojichukulia sheria mikononi..
Awali imedaiwa na
mwendesha mashtaka atuganile msyani kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo mnamo
julai 02 mwaka jana, huko maeneo ya sabasaba manispaa ya morogoro, ambapo bila
halali na akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, alimpiga kwa ngumi maeneo ya
kichwani na tumboni,bahati kabanda maarufu kama masika,aliyekuwa meneja wa baa
yake ya vijana social, na kumsababishia maumivu makali,tukio linalodaiwa
kufanywa baada ya cheka kudaiwa kutoridhishwa na
mahesabu ya mauzo.
Hata hivyo
alipopewa fursa ya kujitetea na mahakama, cheka alishindwa kufanya hivyo na
badala yake kuieleza mahakama kufanya kile itakachokuwa imeamua,na hakimu kumpa
adhabu hiyo ya miaka mitatu jela na akimaliza kifungo alipe fidia ya shilingi
milioni moja kama fidia na malipo ya gharama za matibabu kwa mlalamikaji,
kabanda,hukumu ambayo imezungumziwa na kocha wa cheka saleh komando na mdogo
wake cheka ambaye pia ni bondia cosmas cheka.
Hata hivyo, baada ya hukumu
hiyo, Cheka alidai kwamba sababu halisi ya kifungo ni fitina za viongozi wa mkoa
wa Morogoro baada ya kudai zawadi yake aliyoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete ya
bati.
Cheka aliwaambia Waandishi wa Habari akiwa kwenye gari la Polisi tayari kupelekwa gerezani kwamba, kilichomponza hadi kufungwa leo ni kudai bati alizoahidiwa na Rais Kikwete.
Cheka aliwaambia Waandishi wa Habari akiwa kwenye gari la Polisi tayari kupelekwa gerezani kwamba, kilichomponza hadi kufungwa leo ni kudai bati alizoahidiwa na Rais Kikwete.
Kwa ufupi hadi hukumu hii ya cheka july 5 ndio jeshi la polisi moro lilimshikilia soma.
Tarehe 5 July 2014 Jeshi
la Polisi mkoani Morogoro lilimshilikia bingwa wa ngumi za kulipwa duniani,
Francis Cheka ‘SMG’ kwa tuhuma za kumchapa Meneja wa baa ya Vijana Social Hall
iliyopo Kata ya Sabasaba, Manispaa ya Morogoro.
Kwa mujibu wa maelezo
ya meneja huyo, Bahati Kabanda ‘Masika’ (39), Cheka alifika katika baa hiyo
majira ya jioni na kuanza kumtukana na kumshambulia kwa maneno machafu kisha
kumvamia na kuanza kumchapa ngumi na mateke sehemu za tumboni.
Baa hiyo iilikuwa inamilikiwa
na promota wa ngumi za kulipwa mkoani Morogoro, Zumo Makame.
Kabanda alidai wakati
akipewa kichapo na Cheka, hakuna mtu aliyesogea kuamulia ugomvi huo kutokana na
watu kumuogopa bondia huyo aliyewahi kuwapiga mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Alidai Cheka alifika
katika baa hiyo na dalili za kulewa pombe na baada ya kuondoka, wasamaria wema
walimchukua yeye hadi katika hospitali ya rufaa ambako alilazwa na kupatiwa
vipimo na matibabu ya maumivu aliyoyapata.
Kabanda alidai kuwa
hakuwa na ugomvi na bondia huyo, na hivyo hajui chanzo cha kupigwa na kuongeza
kuwa kama alikuwa na ugomvi nae angemfikisha kwenye vyombo vya sheria na sio
kujichukulia sheria mkononi.
Masika alidai kuwa
pamoja na kupatiwa matibabu, lakini bado hali yake kiafya sio nzuri kutokana na
maumivu aliyoyapata ya mbavu, hivyo kumfanya ashindwe kutembea vizuri.
Baadhi ya mashuhuda
wa tukio hilo walidai kuwa walimuona Cheka akimuangushia kipigo meneja huyo,
lakini walishindwa kuamulia ugomvi huo kutokana na kumwogopa Cheka ambaye ni
bingwa wa ngumi duniani.
Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Ritha Lyamuya, alikiri kumpokea Masika
hospitalini hapo Juni 2, akiwa na maumivu ya mbavu na walipompima X-ray
ilionekana amepata maumivu, hivyo walimpatia matibabu na kumruhusu kurudi
nyumbani.
Alisema hadi
anaruhusiwa hospitalini hapo, Masika alikuwa anaendelea vizuri.
Kamanda wa Polisi
mkoani hapa, Leonard Paulo, amekiri Cheka kufanya shambulio hilo kwa meneja
huyo kwa kumpiga sehemu za tumboni na kichwani.
Paulo alisema Cheka
amekamatwa na anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kwamba katika maelezo
yake, anadai kuwa yeye na Masika walikodi baa hiyo na kufanya biashara kwa pamoja,
lakini baadaye walianza kukosana katika suala na mapato.
Cheka aliendelea
kudai kuwa siku ya tukio alifika katika baa hiyo kwa lengo la kutaka kujua
namna mauzo yanavyokwenda, lakini meneja huyo alimzuia kuingia kaunta na ndipo
ilitokea kutoelewana na baadae ugomvi huo kutokea.
Kamanda Paulo alisema
pamoja na maelezo hayo ya Cheka, lakini ameiagiza timu ya askari kuchunguza kwa
kina tukio hilo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
0 comments:
Post a Comment