Timu ya taifa ya soka
ya Cote d'Ivoire na ile ya Ghana zimefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania
ubingwa wa Afrika, baada ya kupata ushindi jana usiku katika michuano
inayoendela nchini Equitorial Guinea.Mshambuliaji mpya wa Manchester City Wilfried Bonny
aliifungia Cote d'Ivoire mabao 2, huku kabla ya Gervihno kufunga la tatu katika
dakika tisini ya mchuano huo .Cote d'Ivoire ndiyo iliyoanza kupata bao katika
dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza kabla ya El Arbi Soudani kuishawazishia
Algeria katika dakika ya 51, na baadaye Cote d'ivoire kufanikiwa kupata
ushindi.Cote d'Ivoire sasa itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
katika mechi ya nusu fainali ya kwanza siku ya Jumatano Februari 4 katika
uwanja wa Bata.Black Stars ya Ghana nayo ilifuzu baada ya kuifunga Guinea mabao
3 kwa 0.Mabao ya Ghana yalitiwa kimyani na Christian Atsu aliyefunga mabao
mawili na Kwesi Appiah bao moja.Ghana itamenyana na wenyeji Equitorial Guinea
siku ya Alhamisi juma hili katika uwanja wa Malabo.Equitorial Guinea waliweka
historia kwa kufuzu baada ya kuishinda Tunisia mabao 2 kwa 1.Fainali itachezwa
siku ya Jumapili katika uwanja wa Bata.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment