Mapigano yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini Nigeria zikisalia
wiki mbili za uchaguzi wa urais.
Mashambulizi yaliendelea kushuhudiwa Jumapili
Februari 1 katika miji ya Gombe Potiskum, kasazini mshariki mwa Nigeria, huku
mapigano yakiendelea pia kati ya kundi la Boko Haram na majeshi ya Chad na Nigeria
katika miji ya Gamboru na Maiduguri, mashariki mwa nchi.
Mashambulizi hayo katika miji ya Gamboru na
Maiduguri yanasadikiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram, wakati zikisalia
wiki mbili ili uchaguzi wa rais ufanyike.
Wanamgambo wa Boko Haram walianzisha
mashambulizi katika mji wa Maiduguri, ambao ni ngome yao kuu ya zamani, huku
raia wengi wakionwekana katika mji huo baada ya kuyahama makazi yao kufuatia
mapigano yaliyokua yakijiri katika maeneo walipokua wakiishi.
Kwa mujibu wa mashahidi, wanamgambo wa Boko
Haram, ni wengi kaskazini mwa mji wa Maiduguri, na imekua ni vigumu kwa jeshi
la serikali kukabiliana na wanamgambo hao. Wakati huo huo, helikopta za jeshi
la Chad ziliendesha Jumapili Februari 1 mashambulizi ya angani katika ngome za
kundi la Boko Haramkatika mji wa Gamboru. Miji ya Potiskum na Gombe
ilishambuliwa kwa siku hio.
Hayo yakijiri mashambulizi ya kujitoa muhanga
yalishambuliwa katika miji ya Potiskum na Gombe. Watu 7 wameuawa na wengine 7
wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kujitoa muhanga katika miji ya Potiskum na
Gombe katika jimbo la Yobe. Kwa mujibu wa shahidi, mtu aliye jitoa muhanga
alijilipua akiwa ndani ya basi mbele ya nyumba ya Sabo garbu, mfuasi wa chama
tawala, akiwa pia mgombea katika uchaguzi wa Wabunge utakaofanyika Februari 17
Inasadikiwa kuwa wanajeshi 2500 wa Chad
wamewasili nchini Cameroon, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, huku wanajeshi
wengine wakiwa walitumwa kando ya mto el-Beïd, wakiwa na silaha nzitonzito,
kama vifaru, na bunduki zingine za kivita.
0 comments:
Post a Comment