Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
limelaani vikali mauaji ya mwanahabari wa Japan Kenji Goto yaliyofanywa na
kundi la Islamic State IS.
Kwenye taarifa yake, baraza hilo limesema
uhalifu huo unaonesha hatari ambayo waandishi wa habari na watu wengine
wanakabiliwa nayo kila siku nchini Syria.
Baraza
hilo pia limetaka kuachiwa huru kwa watu wengine wanaoshikiliwa na makundi ya
ISIL, AL-Nusra Front pamoja na makundi mengine yenye uhusiano na kundi la
kigaidi la AL-Qaeda.
Baraza hilo pia limeonya mtu au kundi lolote
ambalo litatoa msaada kwa kundi la ISIS kuwa litajumuisha kwenye orodha ya
makundi au watu binafsi wanaotakiwa kuwekewa vikwazo.
0 comments:
Post a Comment