Katibu Mtendaji wa Baraza la Maimamu na Wahubiri
nchini Kenya "CIPK" ameitaka serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha
vazi la hijab ya Kiislamu linaheshimiwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.
Sheikh Mohamed Khalifa
ameongeza kuwa, sharti la hijab ni kusitiri sehemu zote za mwili wa mwanamke,
na wala isimuonyeshe sehemu zake za mwili, na kusababisha matamanio kwa
wanaume.
Sheikh Khalifa aliyasema hayo katika siku ya kimataifa ya kuadhimisha
vazi la hijab, inayofanyika tarehe Mosi Februari kila mwaka na kusisitiza
kwamba, serikali ya Nairobi inapasa kuweka mikakati kabambe ili kuhakikisha
vazi hilo linapewa heshima ipasayo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo. Katibu
Mtendaji wa CIPK ameongeza kuwa, vazi la hijab ni ishara ya stara, faragha na
ucha Mungu kwa mwanamke wa Kiislamu. Hata hivyo, vazi hilo la stara ya mwanamke
wa Kiislamu linakabiliwa na chamgamoto kadhaa ulimwenguni na hasa mashuleni,
vyuoni, makazini na hata kwenye sehemu za umma. Sheikh Khalifa amesema kuwa,
changamoto wanayokumbana nayo wanawake wa Kiislamu ni taasisi za binafsi
zinazohujumu haki zao, kauli iliyoungwa mkono na viongozi wengine wa dini ya
Kiislamu nchini Kenya.
0 comments:
Post a Comment