Na
Anna Nkinda - Lindi
Wakazi wa mkoa wa
Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni
mwa mwaka huu.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Jerry
Silaa wakati akiongea
kwenye kilele cha sherehe za kutimiza miaka 38 ya chama hicho mkoani Lindi zilizofanyika
katika tawi la Mnazi Mmoja
lililopo kata ya Mingoyo wilaya ya Lindi
mjini.
Silaa
mbaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala alisema iwapo mtu atajiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura atashiriki katika uchaguzi mkuu ujao hivyo
basi wakati ukifika ni jukumu la mabalozi
kuwahimiza wananchi kujiandikisha ili wasipoteze haki yao
ya msingi ya kupiga kura.
Aidha
Meya Silaa aliwapongeza wana
CCM kwa ushindi wa asilimia 77 walioupata wakati wa uchaguzi wa Serikali za
mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika
mwishoni mwa mwaka jana na kuwataka kuwa makini katika kuteua viongozi
wanaokubalika na wananchi na
kuachana na makundi yanayokibomoa chama hicho kwa kufanya hivyo itawawezesha kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.
Kwa
upande wa vijana aliwahimiza kujishughulisha katika shughuli za kimaendeleo ili
waweze kujipatia maendeleo kwani mkoa wa Lindi uko katika dira ya
maendeleo kwa kuwa na ardhi
yenye rutuba, barabara nzuri na gesi.
Silaa
alisisitiza, “Nawashauri vijana wenzangu mjiunge
na CCM chama kinachowasaidia
vijana kuwaletea maendeleo ukilinganisha na vyama vingine vinavyowapotezea muda
na kurudisha nyuma maendeleo yenu”.
Alikipatia
kikundi cha Zamira ambchi kinajishughulisha na kilimo na ujasiriamali shilingi
laki tano ili ziweze kuwasaidia kuinua mtaji.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete alisema sherehe hizo zina umuhimu wa
kipekee kwa wana CCM kwani zimeangukia mwaka wenye matukio muhimu na makubwa
kwa nchi ambayo ni kura ya
maoni ya katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais.
Mama
Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema mwaka 2015 ni mwaka wa
kuhitimisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 ambapo Chama hicho
kiliwaomba wananchi wakichague ili kiwafanyie kazi watanzania ambao walikiamini
na kukichagua.
“Matokeo
yake watanzania wameyaona , miundombinu ya barabara, shule na vyuo vimejengwa na watoto wengi hivi sasa wapo
mashuleni. Huduma za afya zimeboreka kwa kujengwa Hospitali, vituo vya afya na
Zahanati”.
Lakini
hata kwa yale ambayo hayakuwepo kwenye Ilani na yalikuwa ni matakwa ya wananchi
chama chetu sikivu hakikusita kuyakubali kwani yalikuwa ni kwa ajili ya maslahi
ya Taifa na vizazi vyetu”, alisema Mama Kikwete.
Kuhusu
Katiba inayopendekezwa MNEC huyo alisema itapigiwa kura ya maoni mwaka huu
mwezi wa nne hivyo basi aliwataka wanaCCM na watanzania wote kwa ujumla
kuipigia kura ya ndiyo katiba pendekezwa kwani inakidhi matakwa ya watanzania
kwa kuwa imegusa katika maeneo yote.
Akiwasalimia
wananchi waliohudhuria sherehe hizo Mkuu wa wilaya ya Lindi Dkt. Nassoro Hamidi
aliwahimiza wazazi kuhakikisha watoto walioandikishwa darasa la kwanza na wale
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaenda shule kuanza masomo ili
waweze kupata elimu itakayowasaidia katika
maisha yao.
Katika
kilele cha sherehe hizo zilizoenda sambamba na wiki ya Chama na Jumuia zake
kauli mbiu yake ni Umoja ni ushindi, Katiba yetu, Taifa letu jumla ya wanachama wapya 448
walijiunga na chama hicho ambapo saba walitoka vyama vya upinzani, Chama cha Wananchi (CUF) watano
na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wawili.
0 comments:
Post a Comment