Waziri wa nchi ofisi ya rais mahusiano na uratibu Dk.MARY NAGU akizungumza na Wananchi wa Singida hawapo pichani.
Baadhi ya kaya maskini mkoani SINGIDA zimepongeza serikali kwa kuanzisha
mpango wa tasaf awamu ya tatu ambao umesaidia kupunguza hali ngumu ya
maisha kwa kuziwezesha kaya hizo kupata mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja
na kugharamia ada na uniform za watoto wao.
Wametoa kauli hiyo kwa waziri wa nchi ofisi ya rais mahusiano na
uratibu , MARY NAGU wakati alipotembelea kaya zinazonufaika na mradi huo
ambapo kwa mkoa wa SINGIDA zaidi ya kaya elfu 42 zinanufaika na mpango
huo.
Mpango huo wa tasaf awamu ya tatu ulizinduliwa mwezi agosti mwaka
2012 na Rais Jakaya kikwete na miaka miwili baadae mkoa wa SINGIDA
uliunganishwa rasmi katika mpango huo ambao mpaka sasa zaidi ya shilingi
bilioni tatu zimekwishatumika .
Takwimu zinaonyesha kuwa Mkoa wa SINGIDA unakaya zaidi ya laki 240 zenye kiwango kikubwa cha umaskini .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment