Naibu Spika wa Bunge JOB NDUGAI amesema fedha nyingi za serikali
hutumika katika kufanya manunuzi mbali mbali katika sekta za umma na
taasisi zake hivyo ni lazima sheria ya manunuzi ikafahamika vema kwa
wataalamu wa manunuzi.
Akizungumza jijini ARUSHA, mara baada yakufungua kongamano la
utawala bora katika ununuzi wa umma lililoshirikisha wakurugenzi na
watendaji,wenyeviti na wajumbe wa bodi pamoja na Mameya na wenyeviti wa
halmashauri nchini,ambaye amesema iwapo manunuzi yasipofanyika vizuri
huweza kusababisha upotevu wa fedha pamoja na mianya ya rushwa.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya udhibiti wa Ununuzi wa Umma nchini Balozi MATERN LUMBANGA,amesema
Changamoto kubwa inayowakabili ni uelewa mdogo kwa wahusika wa ,anunuzi kuhusu sheria ya manunuzi.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamesema upo umuhimu
wakupatiwa elimu kuhusu manunuzi ili kuepusha hasara yakupotea kwa fedha
za umma nchini.
Wajumbe hao wa mkutano wa manunuzi ya umma wanakutana kwa siku TATU
huku wengi wao wakitarajia kupata elimu kuhusu manunuzi sahihi ya umma.
Home
News
Naibu spika wa Bunge NDUGAI asisitiza umuhimu wa kufahamika kwa sheria ya manunuzi kwa wataalamu wa manunuzi
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment