Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameua zaidi ya watu mia moja katika shambulizi lililofanyika dhidi ya mji wa Fotokol nchini Cameroon.
Ripoti zinasema kuwa wapiganaji wa kundi hilo la kitakfiri waliwaua raia waliokuwa katika nyumba zao na ndani ya msikiti mmoja wa eneo hilo.
Watu walioshuhudia wamesema, wapiganaji wa Boko Haram waliingia mji wa Fotokol kupitia Gambaru mapema asubuhi na kuua zaidi ya watu 100 waliokuwa msikitini na majumbani na kuchoma moto mali na milki zao. Askari kadhaa wa Cameroon pia wameuawa katika shambulizi hilo.
Mauaji hayo yamefanyika baada ya viongozi wa nchi za Afrika kuchukua uamuzi wa kuunda kikosi cha majeshi ya nchi kadhaa kwa ajili ya kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram wanaoendelea kufanya uhalifu mkubwa nchini Nigeria na katika nchi jirani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment