Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa kesi za kila wiki za maambikizi ya ugonjwa wa Ebola katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone zimeongezeka katika mwaka mpya wa 2015.Ripoti hiyo imesema kuwa, katika wiki ya mwisho ya mwezi uliopita wa Januari nchi hizo tatu zilikumbwa na ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola na kwamba Shirika la Afya Duniani limethibitisha kesi 124 za maambukizi ya ugonjwa huo katika siku za mwishoni mwa mwezi huo.Nchi za Liberia, Guinea Conakry na Sierra Leone ndizo zilizoathiriwa zaidi na homa hatari ya Ebola. Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonesha kuwa, watu 22 elfu na 92 wameambukizwa virusi hivyo na karibu elfu 9 miongoni mwao wamefariki dunia.Siku chache zilizopita lilianza kutekelezwa zoezi la kutoa chanjo ya Ebola nchini Liberia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment