Image
Image

Mahakama mkoani RUVUMA yazindua magari kwa ajili ya uboreshaji wa mahakama katika utoaji haki


Mahakama Kanda ya SONGEA Mkoani RUVUMA imefanya uzinduzi wa magari madogo aina ya TOYOTA DOUBLE CABIN pamoja na Basi katika Viwanja vya MAHAKAM KUU.
Kutolewa kwa Magari hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Jaji Mkuu ikiwa ni mkakati wa kuboresha huduma za mahakama katika utoaji haki kwa wadau wote wa Mahakama.
Akisoma taarifa kabla ya ufunguzi Mtendaji wa Mahakama kanda ya Songea Mhe. BEATUS BENEDICTUS amesema lengo la kupatiwa magari hayo ni kwa ajili ya kurahisisha huduma katika utoaji haki katika ukaguzi wa Mahakama mbalimbali.
Katika uzinduzi huo Mwanaisha Kwariko JAJI mfawidhi kanda ya Songea amewataka madereva wa magari hayo kuyatunza pia kila mtumishi anawajibu wa kutoa taarifa sehemu husika pale wanapoona kuna matumizi yasiyo sahihi ya magari hayo.
Aidha Mheshimiwa MWANAISHA amesema awali mahakama ilikuwa na uhaba wa usafiri hali ambayo ilikuwa inawapa wakati mgumu wa utendaji kazi kwa wakati.
Magari hayo matano yametolewa kwa kugawiwa katika MAHAKAM ya Wilaya ya Songea, Mbinga , Tunduru , MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa na kwa Mtendaji wa Mahakama.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment