Kamanda IBRAHIM ametoa kauli hiyo kufuatia kukamatwa kwa risasi 524, bunduki moja ya kivita aina ya SMG na Magazini zake tatu katika kizuizi cha POLISI kilichopo katika eneo la NDUTA wilayani KIBONDO zilizokuwa ndani ya HIACE iliyokuwa ikitokea KASULU kuelekea mjini KIBONDO.
Kufuatia kukamatwa kwa Risasi 524, bunduki moja na magazini tatu mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto anayehamia wilayani KALIUA mkoani Tabora anasema suala ulinzi wa nchi Upo mikononi mwa raia wote
Halidhalika kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma JAFARI IBRAHIM wakasema kuwa dhamira ya vizuizi vya polisi ni kudhibiti uhalifu na siyo kuwasumbua abiria ambao wakati mwingine wamekuwa wakilalamika unapofanyika upekuzi kwenye vyombo vya usafiri.
0 comments:
Post a Comment