Mahakama Kuu ya Kenya imetupilia mbali baadhi ya vifungu vya sheria mpya
ya kupambana na ugaidi kikiwemo cha kuvibana vyombo vya habari.
Mahakama hiyo imekitoa kifungu kinachoruhusu kuvichukulia hatua na
kuviadhibu vyombo vya habari endapo vitachapisha habari zinazoelezewa
“kuwa na uwezekano wa kusababisha hofu au hali ya hatari”.
Uamuzi huo
uliotangazwa na Mahakama ya Katiba ya Kenya hapo jana umechukuliwa kuwa
pigo kwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye amekuwa akikabiliwa na mashinikizo
ya kumtaka aimarishe usalama wa nchi baada ya mlolongo wa mashambulio
kadhaa yaliyofanywa ndani ya ardhi ya nchi hiyo likiwemo la mwaka 2013
katika majengo ya maduka ya Westgate jijini Nairobi lililosababisha vifo
vya watu 67.
Muungano wa upinzani na makundi ya kutetea haki za
binadamu yamepinga sheria mpya ya usalama iliyopitishwa mwezi Disemba
mwaka jana yakisema kuwa inakandamiza uhuru wa msingi wa raia.
Licha ya
kutupilia mbali baadhi ya vifungu vya sheria hiyo jopo la majaji watano
wa Mahakama ya Katiba limebakisha kama vilivyo vifungu vingine vingi vya
sheria hiyo kikiwemo kile kinachoruhusu watuhumiwa kushikiliwa kwa muda
wa siku 360 badala ya siku 90 bila kufikishwa mahakamani na kile
kinachowataka wenye nyumba kutoa taarifa za wapangaji wao.
Mwangi
Njoroge, wakili wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema
serikali inafikiria kukata rufani ya kupinga uamuzi huo
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment