Umoja wa Afrika (AU) umeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo ikubali kusaidiwa na vikosi vya Umoja wa Mataifa katika kupambana
na waasi wa mashariki mwa nchi hiyo, baada ya mzozo juu ya tuhuma za
ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya majenerali wa jeshi la Kongo
kuvuruga mpango wa operesheni za pamoja dhidi ya waasi hao.
Vikosi vya
Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Kongo DR vya MONUSCO vilikuwa
vitoe msaada kwa jeshi la Kongo katika operesheni ya kupambana na waasi
wa FDLR, lakini operesheni hiyo ilisimamishwa mwezi huu baada ya
majenerali wawili wa jeshi la Kongo waliokuwa waongoze operesheni hiyo
kutuhumiwa kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu. Rais Joseph Kabila
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alisema wiki iliyopita kwamba
operesheni hiyo ilikuwa imeshaanza bila ya msaada wa vikosi vya MONUSCO.
Baada ya kikao cha wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa
Afrika kilichofanyika hapo jana, mwakilishi maalumu wa AU katika eneo la
Maziwa Makuu Boubacar Gaoussou Diarra, alivieleza vyombo vya habari
kuwa umoja huo unahisi kuna haja ya kufanyika operesheni ya pamoja ili
kuweza kupata mafanikio na kwamba haujafurahishwa na uamuzi wa serikali
ya Kinshasa wa kukataa misaada ya kilojistiki na kitaalamu ya MONUSCO
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment