Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumatatu imeelezea kusambaa na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa ukiukwaji wa haki za kwa misingi ya kidini nchini Iraq na pia kuzorotkwa utawala wa sheria katika sehemu kubwa ya nchi hiyo.
Ripoti hiyo iliyotolewa na mpango wa Umoja wa Mataifa Iraq UNAMI na ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imejumuisha matukio yaliyojiri kati ya Septemba 11 na Desemba 10 mwaka 2014.
Baadhi ya matukio hayo yanayotekelezwa na kundi la kigaidi nchini humo la ISIL ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kimataifa na sheria za kimataifa yakiwemo mauaji ya raia, utekeji nyara, ubakaji, utumwa na usafirishaji haramu wa wanawake na watoto, pia kushinikizwa watoto kuingia vitani, uharibifu wa majengo ya kidini au ya kitamaduni, uporaji na watu kunyimwa uhuru.
Miongoni mwa wanaolengwa kwa maksudi na mashambulizi hayo ya ISIL ni jamii za Turkmen, wakristo wa madehebu ya Shabaks, jamii za Yazidi, waarabi wa madhehebu ya Shia, Wakurdi wa Faili na Kaka'e.
Takribani watu 11, 602 wameuawa na wengine 21, 766 kujeruhiwa kati ya Januari na December 2014.
0 comments:
Post a Comment