Mez B enzi za uhai wake
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini nchini Tanzania Moses Bushagama maarufu kwa jina la Mez B amefariki Dunia leo asubuhi akiwa amelazwa katika hospitali ya mwananchi mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
Mezi B ni msanii moja wapo ambaye alikuwa katika kundi la Chamber Squard ambalo lina undwa na wasanii wengi na hivyo limeanza kuisha baada ya wasanii wake kufariki Dunia.
Akizungumza baada ya kupigiwa simu Dada wa Mez B amethibitisha kifo cha kaka yake ambapo amesema ni muda hivi amekuwa akisumbuliwa wa homa pamoja na tatizo la kuishiwa Damu na hivyo walimpeleka katika hospitali ya GENERAL ambapo hadi jana hali yake haikuwa mbaya sana.
Kwa upande wake mdogo wa marehemu wakati akiongea kupitia simu ya Mkononi huku akiwa anamajonzi na sauti ya simanzi wakati amesema kuwa kaka yake amefariki Dunia akiwa anasumbuliwa na Naimonia ambayo ilikuwa ikimsumbua na kwa muda kidogo hivyo kulazimika kulazwa hospitali mara 4 kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Amesema kuwa hiyo yote ni mipango ya mungu na hivyo wamempoteza kaka yao inauma sana ila haina jinsi ni mipango ya mungu.
Msanii wa mwenzake katika kundi la Chamber Squard Noorah amesema kuwa amepokea taarifa hizo leo asubuhi na siku chache hivi aliongea naye ila malaria ilikuwa ina msumbua ambapo kwa kumbu kumbu zake anasema”Tokea mwezi wa kumi malaria ilikuwa inamsumbua kwahiyo na mm nimeshtushwa na habari hizi za msiba wa Mez”alisema Noora
Aidha nyumbani kwa kina mezi B ni mjini Dodoma kwa taarifa zaidi kuhusu maandalizi mazima tutakufahamisha hapa hapa.Mwenyezi mungu ailaze Roho yake mahala pema amina
0 comments:
Post a Comment