WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema Serikali haijapuuza Sekta ya Elimu nchini, ingawa changamoto ni kubwa ambazo serikali inaendelea kukabiliana nazo.
Alisema hayo baada ya kukagua Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP), sanjari na jengo la kisasa la kumbi la mihadhara katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MUCE), mkoani Iringa.
Pinda alisema serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa katika kuboresha elimu nchini kwa kuimarisha miundombinu na huduma ya utoaji elimu kwa kuanzisha miradi kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu.
“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwenye eneo hili la elimu, hatujapuuza hata kidogo, juhudi ni kubwa na lazima na ninyi mkubali kuwa changamoto zake bado ni kubwa, lakini tunaendelea kuzikabili kwa kadiri ya uwezo wetu,” alisema.
Alisema tofauti na miaka ya nyuma ambayo hali ilionekana kuwa nzuri kiasi, lakini ongezeko la wanafunzi katika vyuo vikuu limechangia kuwapo kwa mahitaji makubwa ya miundombinu katika utoaji huduma.
Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema mradi wa STHEP unahusisha vyuo saba vya Muce, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi, Chuo Kikuu Huria, Chuo Kikuu cha Kilimo (Sua), Chuo Kikuu cha Zanzibar na Duce.
Alizitaja taasisi nyingine ambazo ziko katika mradi huo kuwa ni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (DIT) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
Awali, Naibu Mkuu wa Chuo cha Muce, Profesa William Anangisye alisema mradi wa STHEP unakabiliwa na upungufu wa fedha za kuwasomesha walimu na wataalamu wengine nje ya nchi na pia ukosefu wa samani ili majengo hayo yaanze kutumika.
Home
News
Pinda amesema kuwa serikali haijapuuza sekta ya elimu nchini licha ya changamoto inayo zikabili
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment