Rais museveni ataka majaji kuwahukumu adhabu ya kifo wanaohukumiwa na mashitaka ya mauaji
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewataka majaji nchini humo kuwahukumu adhabu ya kifo watu wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji.
Akifungua mkutano wa 17 wa Majaji jana huko Entebbe, amesema majaji bila ya sababu za msingi wamekuwa hawawashughulikii ipasavyo wauaji, na hutoa adhabu ndogo za vifungo kwa wauaji jambo ambalo linaufanya umma kutokuwa na imani na
mahakama. Rais Museveni ametoa mfano wa wauaji wa kiongozi wa Kiislam Sheikh Abdu Kadir Muwaya wilayani Mayuge na ya kiongozi wa chama cha NRM Tito Okware, wilayani Namayingo, ambapo watuhumiwa walishikiliwa na polisi lakini baadae mahakama iliwaachia
huru.
0 comments:
Post a Comment