Shirika la haki za binaadamu la Amnesty International limezilaumu
serikali ulimwenguni kwa kushindwa kuwalinda mamilioni ya raia dhidi
mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola na makundi yenye silaha.
Ripoti ya mwaka ya shirika hilo imezielezea hatua ambazo
zimechukuliwa na ulimwengu dhidi ya migogoro nchini Nigeria na Syria
kuwa ni za kutia aibu.
Ripoti hiyo imeyalaumu mataifa tajiri duniani kwa kutumia nguvu na
fedha nyingi kuwazuia watu kuingia kwenye mataifa hayo, kuliko
kuwasaidia watu kuishi.
Amnesty International imeuelezea mwaka 2014 kuwa uliokuwa na mauaji
mengi zaidi yaliyofanywa na vyombo vya dola na makundi ya waasi katika
nchi zaidi ya 35 duniani, zikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati na India.
Ripoti hiyo inatabiri kuwa kutakuwa na mauaji na ghasia zaidi katika
mwaka huu, kutokana na kusambaa na kupata nguvu kwa makundi kama Boko
Haram na Islamic state -IS.
Home
News
Shirika la AMNESTY lazitupia lawama serikali kwa kushindwa kulinda raia wake dhidi ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment