Wakati
TANZANIA ikiungana na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya saratani
kila ifikapo February 4 takwimu zinaonyesha hapa nchini zaidi ya asilimia 80 ya
watu wanaogundulika kuugua ugonjwa huo hufariki Dunia ikiwa ni kinyume na viwango
vilivyowekwa na shirika la afya Duniani (WHO) ambapo asilimia 20 ya wagonjwa wa
SARATANI hupoteza maisha kama ilivyo katika nchi zilizoendelea.>>>http://www.itv.co.tz
Takwimu
hizo zinatolewa na waziri wa afya Dk. Seif Rashid ambapo amesema hapa nchini
idadi ya wagonjwa wapya wa saratani kila mwaka ni zaidi ya 34000 huku asilimia
10 tu ndio hufanikiwa kufika hosipitalini kwa ajili ya matibabu ambapo zaidi ya
asilimia 80 hufika wakiwa katika hatua za mwisho ya ugonjwa huo hali
inayopunguza uwezekano wa kupona na kuwataka wananchi ili kuondokana na tatizo
hilo wajenge utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment