Wanawake wameathiriwa kwa kiasi kikubuwa na virusi vya homa ya Ebola amesema Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la masuala ya wanawake katika umoja wa Mataifa , UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka.Katika mahojiano na radio ya Umoja wa Mataifa Bi Phumzile amesema miongoni mwa sababu ni kuwa idadi kubwa ya kundi hilo wako katika sekta ya afya iliyo rasmi na ile isyo rasmi.Hata hivyo kiongozi huyo wa shirika la wanawake katikaUmoja wa Mataifa ametaja hatua zilizochukuliwa na shirika hilo katika mapambano dhidi ya Ebola.“Tumejumuishwa katika ukusanyaji wa taarifa na uangalizi hii ikiwa inamaanisha kufanya kazi na asasi za kiraia katika kila sehemu ya nchi zilizoathiriwa. Pia kukusanya taarifa nyumba kwa nyumba ili kufahamu kwa ukubwa gani wanawake wameathiriwa pamoja na elimu kwa uma.”Liberia, Guinea na Sierra Leone ni nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa kwa wingi na homa ya Ebola
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment