Watumiaji wa teknolojia ya interneti nchini wametakiwa
kutumia teknolojia hii kutafuta taarifa mbalimbali za maarifa na zenye
mwelekeo wa kuleta maendeleo badala ya kutumia teknolojia hii kutafuta
taarifa zisizo na faida na zenye mwelekeo wa kupotosha kizazi cha sasa
kimaadili.
Wito huu umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia,katika siku ya matumizi ya
interneti duniani iliyoadhimishwa leo duniani kote ambako alisema kuwa Vodacom
kama kampuni ya mawasiliano siku zote itakuwa mstari wa mbele kuwaelimisha
wananchi juu ya matumizi bora na sahihi ya mtandao wa interneti.
“Tukiwa kampuni inayoongoza kutoa huduma za mawasiliano
nchini siku zote tutashirikiana na serikali na wadau wengine wa masuala ya
mawasiliano kuhimiza matumizi bora na sahihi ya mtandao wa internet.Matumizi ya
intaneti yamekuwa siyo anasa tena kama ilivyokuwa ikichukuliwa na wengi hapo
awali ambapo watu hujiunga kwa ajili ya kuwasiliana na watu walio nje ya nchi
au kwa burudani nyinginezo. Hivi sasa utumiaji wa intaneti umekuwa kutoka
watu kuwasiliaina mpaka kwa matumizi ya biashara ambapo watu wa mataifa mbali
mbali hukutana mtandaoni kuuza ama kununua bidhaa na huduma,”.Alisema.
Mbali na biashara alisema kuwa interneti imejaa maarifa ya
kielimu ya taaluma mbalimbali ambazo zinafanya dunia kuwa kijiji kimoja hivyo
matumizi mazuri ya interneti yanaweza kumfanya mtu popote alipo kupata taarifa
na maarifa ya fani anayohitaji au taarifa anazotaka kujua kwa haraka na
kwenda na wakati na kuna vyuo vingi duniani vinatoa elimu kwa njia ya mtandao.
“Inashangaza kuona baadhi ya watu hususani katika nchi zetu zinazoendelea
wanatumia muda wao mwingi kuangalia taarifa zisizo na manufaa kwenye mitandao
ya interneti”.Alisema.
Aliwaasa vijana wanaojiita wa kizazi cha Dot.Com hususani
wanafunzi ambao wako mashuleni na vyuoni kuachana na kutumia muda wao kutafuta
taarifa za kuwapotosha na zisizoendana na utamaduni wa kitanzania badala yake
watumie teknolojia hii kupata maarifa na taarifa zenye manufaa kwao na kwa
maisha yao ya baadaye.
Alimalizia kwa kuwahimiza watanzania kujiunga na
mtandao wa Vodacom ambao hivi sasa unatoa huduma ya interneti yenye kasi kubwa
na viwango vya gharama nafuu lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha idadi ya
watumiaji wa interneti nchini inaongezeka ili kwenda na nchi zilizopo katika
ukanda wa Afrika Mashariki.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment