Taasisi ya maendeleo ya VICTORIA FOUNDATION ya mkoani GEITA imekabidhi
vyerehani Kumi kwa chama cha watu wenye ulemavu mkoani humo ili
kukiwezesha chama hicho kubuni mradi wa ushonaji nguo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vyerehani hivyo Mkuu wa wilaya ya
GEITA - MANZIE MANGOCHIE ametoa wito kwa taasisi nyingine nchini
kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
Vyerehani hivyo vimekabidhiwa kwa kikundi cha walemavu mkoani geita
na mkuu wa wilaya ya geita MANZIE MAGOCHIE na kutoa changamoto kwa kwa
taasisi nyingine kuwasaidia watu wenye ulemavu.
Kwa upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu mkoani geita hawakusita kuonyesha furaha yao baada ya kukabidhiwa vyerehani hivyo.
Katika hafla hiyo watu wenye ulemavu mkoani geita pia walipata fursa
ya kujumuika katika chakula cha mchana walichoandaliwa na taasisi ya
maendeleo ya victoria foundation.
Home
News
Watu wenye ulemavu mkoani GEITA wapokea msaada wa vyerehani ili kubuni mradi wa ushonaji nguo na kujikwamua kimaisha
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment