Ametoa pongezi
hizo jana usiku (Jumanne, Februari 24, 2015) wakati akizungumza na viongozi wa
mkoa huo na wilaya zote wakiwemo wadau mbalimbali na viongozi wa dini mara
baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Mbeya.
Alisema katika
mipango yake, Serikali ililenga kwamba pato la mtu kwa mwaka liwe sh. 1,186,
200, lakini kwa sababu ya jitihada mbalimbali mkoa huo umelivuka.“Katika
taarifa aliyonisomea, Kaimu Mkuu wa Mkoa amesema wastani wa pato la mwananchi
umeongezeka kutoka sh. 711,201/- mwaka 2008 hadi kufikia sh 1,420,427/- mwaka
2013 na kwamba mkoa unachangia asilimia 7.43 ya Pato la Taifa,” alisema.
Alisema kipato
cha mtu mmoja kwa siku ni sh. 3,891/- ambazo ni zaidi ya Dola mbili za Marekani
(sh. 3,400/-). “Wakubwa hawa wanatupima kwa kuangalia kipato cha mtu kwa siku.
Wanasema nchi ni maskini iwapo watu wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku
(sawa na sh. 1,700/-).”
“Mbeya imeendelea
kushika nafasi ya tatu kwa kuchangia vizuri Pato la Taifa ikiwa imetanguliwa na
Dar es Salaam na Iringa. Ninawapongeza kwa sababu mmevuka malengo ya Taifa
katika eneo la pato la mtu mmoja mmoja,” alisema Waziri Mkuu.
Mapema, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Deodatus Kinawilo ambaye
pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, alisema pato la mkoa limeongezeka kutoka sh.
trilioni 1.779 mwaka 2008 na kufikia sh. trilioni 3.951 mwaka 2013.
“Uchumi wa mkoa
huu unategemea kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, uvunaji mazao ya maliasili,
biashara, uzalishaji viwandani na ajira katika taasisi za serikali na sekta
binafsi,” alisema.
Wakati
huohuo, uongozi wa mkoa wa Mbeya umetakiwa kuongeza bidii ili uweze
kuinua kiwango cha ufaulu wa elimu ya kwa sababu umekuwa ukiendelea kushuka na
kuwa chini ya kiwango cha asilimia 60 kilichowekwa na Serikali.
Waziri Mkuu
aliutaka uongozi huo ubuni mbinu za kisomi zitakazowawezesha wanafunzi wa shule
za msingi kuelewa wanachofundishwa, hivyo, kufaulu mitihani yao vizuri. ”Ufaulu
wenu kwa shule za msingi ni asilimia 46.6, uko chini ya kiwango cha kitaifa cha
ufaulu kwa asilimia 13.4. Ni matokeo yasiyoridhisha, fanyeni utaratibu maalum
ili yapande,” alisema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 25, 2015.
0 comments:
Post a Comment